LIGI YA MABINGWA ULAYA : PSG VS BARCELONA NI SHIDAAAH!!!
Katika uwanja wa Parc Des Princes jijini Paris leo litapigwa bonge moja la mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kati ya wenyeji Paris Saint German na FC Barcelona kutoka Spain katika raundi ya pili ya mechi za makundi katika kundi F.
Matajiri PSG wataingia dimbani wakimkosa mshambuliaji wao Zlatan Ibrahimovic ambaye pengine anaweza asicheze dhidi ya klabu yake hiyo ya zamani kutokana na kuwa majeruhi ya kisigino.
Ibrahimovic aliisaidia Barcelona kushinda La Liga mara moja, Spanish Super Cup mara moja,UEFA super cup mara moja na Club World Cup mara moja alupojiunga na Barca mwaka 2009 akitokea Inter Milan.
PSG walitoka sare katika mechi za ufunguzi dhidi ya Ajax ugenini wakati Barcelona wao waliifunga Bate nyumbani bao 1-0.
Bqrcelona wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa katika kiwango bora katika ligi ya Spaun wakiwa wanaongoza ligi huku wakiwa wameshafunga magoli 17 na kufungwa moja tu.
Andres Iniesta atacheza mchezo wake wa 100 leo katika ligi ya mabingwa Ulaya akiwa na Barcelona.
Mara ya mwisho kukutana timu hizo zilitoka sare ya 1-1 katika dimba la Camp Nou nyumbani kwa Barcelona.
RATIBA KAMILI YA MECHI ZA LEO NI KAMA IFUATAVYO
GROUP E
19:00 CSKA Moscow vs Bayern Munich
21::45 Man City vs AS Roma
GROUP F
21:45 APOEL vs Ajax
21:45 PSG vs Barcelona
GROUP G
21:45 Schalke 04 vs Maribor
21:45 Sporting vs Chelsea
GROUP H
21:45 BATE vs Athletico Bilbao
21:45 Shaktar vs FC Porto
NOTE: MUDA NI KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI
{ Edo Daniel Chibo}
No comments