LIGI KUU TANZANIA BARA - AZAM YATAKATA, YANGA ISHALIZWA MORO



Ligi kuu Tanzania Bara inaendelea katika viwanja 6 nchini ambapo mpaka saa ikiwa ni mapumziko katika viwanja vingi huku Azam FC wakionekana kutakata wakati Yanga wao hali ngumu Huko Morogoro.

Mwandishi wetu Allen Kaijage aliyoko Chamazi anaripoti kuwa mabingwa watetezi Azam FC wanaongoza kwa bao 2-0 dhidi ya Polisi Morogoro magoli yakifungwa na Didier Kavumbagu dakika ya 14 akipokea pasi ya Kipre Tchetche huku goli la Pili likifungwa na Aggrey Morice pasi ikitokea kwa Kipre Tcheche tena.



Azam FC wameonekana kuimarika na kuwadhibiti vilivyo Polisi na pengine kipindi cha pili magoli yakaongezeka.

KUTOKA Morogoro tunaarifiwa kuwa goli la Dakika ya 15 la mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Mussa Hassan Mgosi linawapa Mtibwa uongozi wa bao 1-0 mpaka mapumziko dhidi ya Yanga SC ambao leo wameshusha silaha zao zote akiwemo Jaja,Ngasa,Niyonzima na Kiiza.

.....Endelea kufatilia hapa tutakupa matokeo kadri titakavyoyapata.

No comments

Powered by Blogger.