HIVI ANKO HAO JAMAA MBAKUSHOBOROLA BATAI?
Hakuna kitu kigumu kama kufanya
uchaguzi wa vitu vichache katika vingi. Ili kufanya uchaguzi sahihi wanauchumi
hutumia kanuni inayoitwa “scale of
preference” (kuchagua kitu au vitu katika vitu vingi kutokana na umuhimu wa
mahitaji yako) Kwenye “scale of
preference” utafanya uchaguzi kuanzia kwenye kitu muhimu kabisa halafu
vingine hufuata. Kama unataka kuchagua bidhaa lazima uchague kulingana na mahitaji
yako muhimu halafu bidhaa kwa ajili ya mahitaji ya ziada zitafuata.
Hata kwenye uchaguzi wa marafiki na wasaidizi lazima tutumie kanuni hii ya wachumi. Ukitaka kuchagua marafiki lazima upime umuhimu wa hao watu unaotaka kuwafanya rafiki zako. Sasa hapo kila mtu huwa na uhitaji wake. Utachagua rafiki kutokana na sifa za uhitaji wako. Mwenye sifa za kutosha ndio utampa kipaumbele.
Vivyo hivyo kwenye kuchagua wasaidizi wa kazi lazima uwachague watu
kutokana na kazihusika. Huwezi kumchagua daktari kwenye kazi ya ujenzi kisa
huyo daktari ni mchapa kazi hospitali, Au umchague mwalimu kwenye kazi ya uhasibu
kwasababu tu mwalimu huyo unamfahamu. Hapo utajikaanga kama nguruwe. Kwani
mwalimu hawezi kukupa ushauri mzuri wa maswala ya fedha kama muhasibu
aliyesomea uhasibu pia daktari hawezi kukupa ushauri mzuri wa maswala ya ujenzi
kama atakavyokupa mhandisi.Hata kwenye uchaguzi wa marafiki na wasaidizi lazima tutumie kanuni hii ya wachumi. Ukitaka kuchagua marafiki lazima upime umuhimu wa hao watu unaotaka kuwafanya rafiki zako. Sasa hapo kila mtu huwa na uhitaji wake. Utachagua rafiki kutokana na sifa za uhitaji wako. Mwenye sifa za kutosha ndio utampa kipaumbele.
Hapa ndipo Watanzania wengi tunafeli, mara nyingi hatufanyi uchaguzi sahihi. Watu wengi tumeweka wasaidizi wa kazi wasio na ujuzi mkubwa kwenye kazi husika. Watu wengi wameweka undugu na urafiki mbele katika kazi ndio maana hatuendelei. Mtu anafanya kazi
kwasababu bosi wake ni Mtoto wa baba yake mdogo. Sikatai kumuweka mtu kwasababu ni ndugu yako au rafiki yako, Bali nakataa uwepo wa ndugu au rafiki asiye na taaluma ya kutosha kwenye kazi anayoenda kuifanya wakati huo huo wapo watu wenye ujuzi mkubwa wa kufanya kazi hiyo.
Dhambi hii ipo kwenye kila sekta nchini. Hivi juzi tu tumetoka kusikia kusitishwa kwa ajira za uhamiaji kutokana na mambo haya haya. Nchi yetu aiendelei kutokana na kukosa watu sahihi wakutuongoza, Baba Mwanaasha anaweza kuwa na mipango mizuri juu ya nchi yetu lakini watu wanaomzunguka wakawa wanamkwamisha. Nimejiuliza kwanini michezo yetu aiendelei nikagundua tatizo ni hili hili. Tumekosa watu sahihi wa kuongoza michezo yetu. Si riadha wala mpira wa mikono, mambo ndiyo yale yale kila siku tumekuwa watu wa kushindwa. Huku kwenye mpira wa miguu ndiyo kabisaa kila siku afadhali ya jana.
Anko anaweza akawa na maono mema na soka letu lakini tatizo likawa kwa watu aliowaweka karibu. Sijui wanamshauri nini anko watu hawa? Anko, watu hawa ndio wanakukwamisha na kukwamisha soka letu kwa ujumla. Sawa anko, najua ufanyi kazi peke yako ila nakulaumu kwa kukimbia kitu kinachoitwa 'scale of preference'. Anko umenifanya nimkumbuke mzee Johnson Mbwambwo, Mzee Johnson Mbwambwo ambaye ni muandishi mashuhuri wa habari za siasa alishawai sema maneno haya "Watawala wengi duniani hasa wa nchi zetu za Afrika wanapenda mno kuzungukwa na watu (walamba miguu) ambao unaweza kuwaita court jesters au hata sycophants. Kwa kawaida watu hawa kazi yao ni kusifia kila kitu raisi anachokifanya au kukitamka, na wanafanya hivyo ili wampendezeshe na aone kuwa watu wanampenda. Raisi akicheka wao watacheka zaidi, Raisi akinuna wao wananuna zaidi, Rais akimkasirikia mtu, wao humkasirikia mtu huyo zaidi. Raisi akitukana wao hutukana zaidi. Ni Court jesters hao ambao kihulka unaweza kuwaita Sycophants.”
Anko nahisi kuna “court jesters” wanakutafuna
na kukurudisha nyuma. Anko ungekuwa na washauri wazuri tusingekua tunahesabu
siku zetu za nyuma. Anko leo mnapanga hiki kesho mnatengua si utoto huo. Anko leo
nataka nikueleze mambo mawili kati ya mengi niliyonayo ambayo walibidi wafanye
washauri wako wa karibu ambao ni viongozi wenzako wa shirikisho.
La kwanza ni hilo nililoanza
kuligusia hapo juu. Anko awali mliweka agosti 3 kuwa mwisho wa usajili mkasogeza
mbele mpaka agosti 17, mkaona haitoshi mkaongeza tena siku na mpaka ukafika
mwezi september. Anko hapa napata wasi wasi mkubwa na watu wanaokuzunguka. Huu
uswahili mpaka lini? Kwanini kila siku sisi tu? Kama tumeshindwa kusimamia
jambo hili dogo tutaweza kweli kusimamia mashindano makubwa unayoyaota ukiwa
macho?
Anko kubwa na la msingi tulitarajia
utatengeneza shirikisho jipya lisilo na chembe ya ukanjanja lakini majanga ni
yale yale tena yanaendelea kuzidi. Anko nilitarajia shirikisho lako litajitenga
na siasa za simba na yanga lakini haipo hivyo. Miaka michache iliyopita
tulishuhudia usajili wenye utata wa Athuman Iddi ‘chuji’, Kelvin Yondani na
Mbuyu Twite na sasa Emmanuel Okwi. Kanuni za usajili zipo lakini hazifuatwi. Hapa
ndipo napata wasi wasi mkubwa na watendaji wa TFF, Kuna kipindi kanuni
ziliwekwa pembeni na mchezaji akaamuliwa acheze timu fulani kwa kupiga kura. Hii
inatokea Tanzania tu. Anko mtazibeba simba na yanga mpaka lini? Kwanini kila
siku ni wao tu? Au shirikisho letu halina kanuni zake bali linaongozwa na
kanuni za simba na yanga?
Anko hao jamaa “mbakushoborola batai?” (wanakushauri nini) Anko labda nikiuliza kwa
lugha hii utajua nimemaanisha nini. Labda na hao jamaa wataelewa
nnachozungumza. Anko bado una muda mwingi pia unao muda wa kufanya mabadiliko
ya jamaa zako bila kujali ni rafiki au ndugu zako, kuna watu wa mpira wengi
sana wanaweza kurekebisha madudu wanayofanya washauri wako wa sasa. Anko fanya
hima watanzania wamechoka kusubiri. Usipofanya mabadiliko wataomba
kukubadilisha.
Allen kaijage
0655106767
kaijagejr@gmail.com
No comments