FERNANDINHO NA FERNANDO - UKIWAONA WAMEFANANA LAKINI KILA MMOJA ANALIPWA KUTOKANA NA MGUU WAKE


Moja ya sababu kubwa iliyomfanya kocha wa Mabingwa wa Ligi kuu England Manuel Pelegrin kuingia sokoni na kuimarisha safu yake ya kiungo ni kuona ni namna gani watakavyoweza kumkabili mpinzani wake yeyote watakayekutana naye.
 Na hapa ndipo anapoingia mfukoni na kuleta wachezaji ambao ni wachezaji walio juu katika uchezaji. Kiukweli Man City wamekamilika na wana kikosi kipana sana ambapo katika kila idara kuna zaidi ya wachezaji wawili wanaocheza katika nafasi hiyo.



Hebu tuwaangalie hawa wachezaji wawili ambao ni FERNANDINHO na FERNANDO mimi binafsi sikuelewa sababu za undani zaidi ya kwa nini
Kocha Manuel Pelegrin aliamua kumleta FERNANDO kwa tayari alishakua na FERNANDINHO na akina James Milner lakini sasa nimegundua kuwa kila mmoja
ana kitu fulani zaidi ya mwenzake.

FERNANDO na FERNANDINHO wote asili yao ni kiungo wakabaji (holding mildifielders) pale katikati ya kiwanja lakini FERNANDINHO ana kitu cha ziada zaidi kwani anaweza kucheza pia kama kiungo mshambuliaji tofauti na  FERNANDO ambaye katika kushambulia sio mzuri sana ila katika kukaba na kuzuia ni mzuri kidogo zaidi ya FERNANDINHO

Takwimu zinaniambia kuwa katika ligi kuu nchini Ureno msimu wa 2012/2013 FERNANDO alikuwa ni kiungo Aliyecheza faulo nyingi kuliko viungo wote katika ligi hiyo na hapa ndipo ninapoelewa kwa nini Pelegrin ameamua kumwamini zaidi FERNANDO kuliko FERNANDINHO nia na kusudi ikiwa ni kumpa nafasi zaidi Yaya Toure kushambulia zaidi akitokea katikati ya kiwanja zaidi ya msimu uliopita.

Katika kikosi una wachezaji watatu walio katika kiwango bora kabisa tena katika nafasi ya kiungo unategemea nini?
Ubingwa ni zaidi ya 80% kwa Man City

 KWELI WAMEFANANA LAKINI KILA MMOJA ANALIPWA KUTOKANA NA MGUU WAKE!!!

.... Imeandikwa na Fahim Wasso toka katika kundi la Wapenda Soka (Kandanda) facebook.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.