THE TRUE RED DEVILS

KIKOSI CHA MABINGWA WA KWANZA EPL 1992/1993 - MANCHESTER UNITED

Wakati Ligi ya daraja la juu nchini Uingereza ikianzishwa mwaka1888 timu ya PRISTON NORTH END Iliibuka bingwa wa kwanza kwa kucheza michezo yote bila kufungwa na kuweka rekodi iliyokuja kuvunjwa miaka zaidi ya 100 na Arsenal mwaka 2004 lakin Tangu kuanza kwa ligi kwa mfumo mpya msimu wa mwaka 1992/1993 ikijulikana kama English Premier Legue (EPL) Man United ndo imekua bingwa wa kwanza na Tangu mwaka huo mpaka leo imekua ndo timu iliyoongoza kwa kuchukua kombe hilo mara nyingi kuliko timu zote sio tu kwa miaka hii 20 lakini kwa miaka yote ikichukua mara 19 huku mara 12 ikiwa ni tangu msimu huo wa 1992/1993.

THE TRUE RED DEVILS leo inaangalia wachezaji walioisaidia Man United kuibuka bingwa katika msimu huo wa kwanza na kikosi gani tulichonacho katika msimu huu wa 2012/2013.
MABINGWA WA KWANZA WA EPL
Katika picha wanaonekana wachezaji wote wa kikiosi cha Mabingwa wa kwanza wa EPL katika picha na majina yao ni kama yafuatavyo:

Mstari wa kwanza nyuma: Andrei Kanchelskis, Mike Phelan, Eric Cantona, Peter Schmeichel, Les Sealey, Gary Pallister, Dion Dublin, Lee Sharpe.

Mstari wa katikati : Norman Davies (meneja wa vifaa), Brian McClair, Denis Irwin, Ryan Giggs, Lee Martin, Darren Ferguson (mtoto wa Sir Alex Ferguson), Roy Keane, Mark Hughes, Jim McGregor (daktari wa timu).

Mstari wa mbele: Danny Wallace, Clayton Blackmore, Sir Alex Ferguson(kocha mkuu) Steve Bruce, Bryan Robson, Brian Kidd (Kocha msaidizi), Paul Ince, Paul Parker.

Hiki ndo kikosi kilichoweka historia huku ikiwa na mchezaji mmoja tu ambaye bado anaichezea Man United mpaka sasa Ryan Giggs na wengi wa wakali hawa hivi sasa ni makocha wa timu mbalimbali barani Ulaya

                          WAKO WAPI WAKALI HAO?
  • Andrei Kanchelskis hivi sasa anaifundisha timu ya FC UFA ya Russia
  • Michael Christopher "Mike" Phelan kila mmoja anamfahamu huyu jamaa kwani ni kocha msaidizi wa kikosi cha sasa cha United akimsaidia SAF
  • Eric Cantona hivi sasa ni muigizaji wa movies nchini Ufaransa
  • Peter Schmeichel msimu huo wa mwaka 1992/1993 alikua kipa bora duniani hivi sasa amestaafu soka akiendelea kula mafao yake.
  • Les Sealey alikua golikipa msaidizi ambae alifariki mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 43 (R.I.P)
  • Gary Pallister hivi sasa huyu jamaa ni mchambuzi wa maswala ya soka katika vituo vya luninga
  • Dion Dublin beki huyu raia wa Uingereza hivi sasa amestaafu maswala ya soka
  • Lee Sharpe winga ya kushoto ya Man United ilikamilishwa na huyu jamaa wakati huo Ryan Giggs akianzia benchi hivi sasa Lee Sharpe ni mchambuzi wa maswala ya soka.
  • Brian McClair hivi sasa huyu jamaa ni mkurugenzi wa soka la vijana katika timu ya Man United
  •  Denis Irwin beki kisiki huyu raia wa Ireland akiwa na umri wa miaka 47 hivi sasa alistaafu kucheza mpira tangu mwaka 2004 na hivi sasa yupo tu na familia yake
  • Ryan Giggs akiwa na umri wa miaka 39 hivi sasa bado anaichezea Man United katika msimu wake wa 22 katika klabu hii.

  • Lee Martin beki wa kushoto huyu raia wa England ambaye alifunga goli pekee katika fainali ya kombe la  FA dhidi ya Crystal Palace mwaka 1991
  • Darren Ferguson huyu ni mtoto wa Kocha Alex Ferguson ambaye kwa sasa Darren anakinoa kikosi kinachopigania kutoshuka daraja katika ligi daraja la kwanza England maarufu kama Championship timu ya Peterborough United
  • Roy Keane ni mmojawapo wa manahodha waliopita United kwa mafanikio makubwa hivi sasa hana timu ya kuifundisha ila amewahi kuzifundisha Sunderland na Ipswich Town
  • Mark Hughes mmojawapo wa washambuliaji wakali kutokea katika kikosi cha Man United ana umri wa miaka 49 hivi sasa ni kocha aliyetimuliwa kukinoa kikosi cha QPR na nafasi yake kuchukua Harry Rednapp
  • Danny Wallace huyu amestaafu soka
  • Clayton Blackmore ni kati ya wachezaji walioingia katika fani ya ukocha akiwa kocha mkuu wa timu ya Porthmadog
  •  Steve Bruce ana umri wa miaka 52 hivi sasa na ni kocha wa timu inayopigania kupanda daraja na kucheza EPL msimu ujao Hull City.
  • Bryan Robson huyu ni kati ya makapteni walioitumikia United kwa kipindi kirefu kuzidi wote akijiunga na United mwaka 1981. Alistaafu kucheza soka mwaka 1997 akiwa na klabu ya Middlesbrough wakati huo akicheza kama kiungo wa kati. Amekua kocha kwa kipindi kirefu ikiwa pamoja na kuifundisha timu ya Taifa ya Thailand. Hivi sasa ameteuliwa kama balozi wa heshima wa klabu ya Man United.
                                                                Robson
  • Paul Ince huyu jamaa ni rafiki mkubwa wa Roy Keane ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya daraja la kwanza England, Blackpool.
  • Paul Parker beki huyu raia wa England ana miaka 43 amestaafu kucheza soka na hivi sasa amejikita katika uchambuzi wa maswala ya soka katika vituo vya luninga.

Hiki ndicho kikosi cha mabingwa wa kwanza wa Ligi kuu nchini England (EPL) huku kocha mkuu akibaki yule yule Sir Alex Ferguson ambaye bado anakifundisha kikosi cha sasa cha United.

Katika kikosi cha sasa cha Man United kimesheheni vijana wengi na hii ndo listi ya majina ya wachezaji wa Man United katika msimu huu ambao tunaelekea kutawazwa kua mabingwa mara 20 wa ligi Soka nchini England kama ilivyotayarishwa na ABEL CHIMWEJO kutoka katika kundi la WAPENDA SOKA (KANDANDA) katika mtandao wa Facebook.

WACHEZAJI WA MAN UNITED MSIMU HUU 2012/2013, MAMENEJA NA JOPO LA MAKOCHA

WACHEZAJI:
1.David De Gea
2.Rafael da Silva
3.Patrice Evra
4.Phil Jones
5.Rio Ferdinand
6.Jonny Evans
7.Antonio Valencia
8.Anderson
10.Wayne Rooney
11.Ryan Giggs
12.Chris Smalling
13.Anders Lindegaard                                            
14.Javier Hernandez
15.Nemanja Vidic
16.Michael Carrick
17.Nani
18.Ashley Young
19.Danny Welbeck
20.Robin Van Persie
21.Angelo Henriquez(on loan)
22.Paul Scholes
23.Tom Cleverley
24.Daren Fletcher
25.Nick Powell
26.Shinji Kagawa
27.Federico Macheda(yuko kwa mkopo katika klabu ya Sturtgat ya Ujerumani)
28.Alexander Büttner
33.Bebe(Yuko kwao Ureno kwa mkopo)
38.Michael Keane(on loan)
40.Ben Amos
50.Sam Johnstome
Fabio da Silva(Yuko QPR kwa mkopo)

Wengine:
Luke McCullough
Marnick Vermijl
Tom Thorpe
Tyler Blackett
Sean MacGinty
Fredric Veseli
Larnell Cole
Jesse Lingard
Will Keane

WALIOKO NJE YA UNITED KWA MKOPO NI :
Joh Cofie
Wilfried Zaha
Scott Wootton
Reece Brown
Davide Petrucci

KWA LEO TUNAISHIA HAPA TUKUTANE WIKI IJAYO KATIKA THE TRUE RED DEVILS NYINGINE
Imetayarishwa na kuhaririwa na Edo Daniel Chibo kwa msaada wa wadau kadhaa akiwemo Abel Chimwejo
Kwa maoni,Ushauri usisite kunitumia katika mfalme.edo@gmail.com au nicheki hewani katika 0715 12 7272 na Edo Daniel Chibo katika ukurasa wa Facebook.

2 comments:

Powered by Blogger.