MIWANI PANA YA EDO KUHUSU UWANJA WA ALLY HASSAN MWINYI - TABORA
Wakati dunia ikitafuta maeneo ya Uwekezaji hapa kwetu Tanzania ni tofauti kwani tuna maeneo mengi ambayo hatuyatumii.
Mfano mzuri ni pale unaposafiri na kukuta mapori kibao njiani Wakati hapa Dar Tukibanana eti hakuna maeneo hata ya kujenga choo na kama yapo basi hupatikana kwa ghaama kubwa.
Vivyo hivyo sekta ya michezo imekumbwa na balaa hilo kwani Miundo mbinu mingi imekua ikichezewa,kubomolewa kama pale Jangwani na pengine kutelekezwa kama viwanja vingi vingi Mikoani.
Mwaka 2008 Nilitembelea Shinyanga na nikawa na shauku kubwa kuushuhudia uwanja wa Kambarage kwa Sifa nilizozisikia kipindi nasoma wakati timu kama Kahama United wakitumia Uwanja huo mechi kubwa dhidi ya Yanga na Simba.
lakini looooh! niliyoyakuta yanasikitisha uwanja umegeuka kua kama makubusho ya Taifa ( Sina uhakika kama wameshafanya ukarabati Tangu mwaka huo kwani sijatimba tena hapo)
Miwani yangu pana leo imejikita katika kuangazia miundo mbinu katika michezo na hapa ningetamani kutumia ndege ya bei rahisi ya Fast Jet nikatua Chimbuko la viapaji vingi vya soka akiwemo Kiungo Bora kabisa Tanzania Haruna Moshi Boban
Yeeeeeeees!!!!!!! Naizungumzia TABORA hapa na zaidi ya yote nauzungumzia uwanja maarufu wenye kuingiza Mashabiki pamoja na vyombo vyao vya usafiri.
Huu ni moja kati ya viwanja vingi vinavyomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi C.C.M
Ni maajabu mengine nchi hii kwa Vilabu vya mpira na Chama cha Mpira kutokua na viwanja vya mpira lakini Chama Cha siasa kikamiliki viwanja karibia 80% nchi nzima hii ni hatari kwani ipo siku anaweza kutokea kiongozi digteta asiyependa michezo akaamua kubomolewa viwanja hivi na mwishowe tukabaki bila viwanja.
Itakua ngumu sana kwa Mtu yeyote kuvichukua hivi viwanja mikononi mwa CCM kwani wana mikataba inayowalinda wakati viwanja vikijengwa na haijalishi kama mikataba hiyo ilikua chini ya chama kimoja au lah lakini jina la mikataba bado ni la CCM.
Hali ya Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi kwa majengo ni mbaya kwa sasa kama inavyoonekana katika picha japokua ni kati ya viwanja bora zaidi katika nchi hii ukiacha Taifa,Uhuru na CCM Kirumba pale Mwanza.
Historia inasema ujenzi wa uwanja huo ulitokana na Wananchi kuchangia nguvu zao kiihari na hata kilazima mpaka Uwanja ulipokamilika kwa ahadi kwamba uwanja huo ni wa kisasa na itakua chanzo kikubwa cha mapato kwa Mkoa japokua sina uhakika kama lengo hilo limetimia ila nijuavyo sasa CCM wanapata mapato kwa kila shughuli inayofanyika hapo.
Uwanja huo upo katikati ya mji wa Tabora, Mji unaosifika kua na Utajiri wa Wachezaji waliowahi kuwika akiwemo Idd Moshi na haruna Moshi "Boban"
Polisi na Rhino Rangers za Tabora zinazoshiriki ligi ya daraja la kwanza Taifa zinautumia uwanja huo kwa sasa ambapo tabora haina timu inayoshiriki ligi kuu ya Vodacom.
Ally Hassan Mwinyi ni kati ya Viwanja vingi vilivyotelekezwa hapa Tanzania na hii inatokana na vyama vya mikoa kushindwa kutengeneza program za mikoa husika katika kuendeleza soka.
Miwani yangu pana itaendelea kuvumbua yote yasiyoonekana mpaka kutumia Big lens kama yangu kuyasema.
Ukiwa kama Mpenda soka Unadhani nini kinapaswa kufanyika katika viwanja hivi?
,,,,,,,,,,,,,"""" Merry Christmass kwenu Wapenda Soka"""""",,,,,,,,,,
Asante kwa Abel Chimwejo wa wapenda Soka Group kwa kunisaidia kuzipata picha za uwanja huo kwasasa.
Tuonane wakati mwingine na kwa maoni tuwasiliane
wapendasoka@gmail.com au nicheki hewani 0715 12 72 72
Mfano mzuri ni pale unaposafiri na kukuta mapori kibao njiani Wakati hapa Dar Tukibanana eti hakuna maeneo hata ya kujenga choo na kama yapo basi hupatikana kwa ghaama kubwa.
Vivyo hivyo sekta ya michezo imekumbwa na balaa hilo kwani Miundo mbinu mingi imekua ikichezewa,kubomolewa kama pale Jangwani na pengine kutelekezwa kama viwanja vingi vingi Mikoani.
Jukwaa kuu la uwanja wa Ally Hassan Mwinyi |
Mwaka 2008 Nilitembelea Shinyanga na nikawa na shauku kubwa kuushuhudia uwanja wa Kambarage kwa Sifa nilizozisikia kipindi nasoma wakati timu kama Kahama United wakitumia Uwanja huo mechi kubwa dhidi ya Yanga na Simba.
lakini looooh! niliyoyakuta yanasikitisha uwanja umegeuka kua kama makubusho ya Taifa ( Sina uhakika kama wameshafanya ukarabati Tangu mwaka huo kwani sijatimba tena hapo)
Miwani yangu pana leo imejikita katika kuangazia miundo mbinu katika michezo na hapa ningetamani kutumia ndege ya bei rahisi ya Fast Jet nikatua Chimbuko la viapaji vingi vya soka akiwemo Kiungo Bora kabisa Tanzania Haruna Moshi Boban
Yeeeeeeees!!!!!!! Naizungumzia TABORA hapa na zaidi ya yote nauzungumzia uwanja maarufu wenye kuingiza Mashabiki pamoja na vyombo vyao vya usafiri.
UWANJA WA ALLY HASSAN MWINYI - TABORA
Huu ni moja kati ya viwanja vingi vinavyomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi C.C.M
Ni maajabu mengine nchi hii kwa Vilabu vya mpira na Chama cha Mpira kutokua na viwanja vya mpira lakini Chama Cha siasa kikamiliki viwanja karibia 80% nchi nzima hii ni hatari kwani ipo siku anaweza kutokea kiongozi digteta asiyependa michezo akaamua kubomolewa viwanja hivi na mwishowe tukabaki bila viwanja.
Itakua ngumu sana kwa Mtu yeyote kuvichukua hivi viwanja mikononi mwa CCM kwani wana mikataba inayowalinda wakati viwanja vikijengwa na haijalishi kama mikataba hiyo ilikua chini ya chama kimoja au lah lakini jina la mikataba bado ni la CCM.
Hali ya Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi kwa majengo ni mbaya kwa sasa kama inavyoonekana katika picha japokua ni kati ya viwanja bora zaidi katika nchi hii ukiacha Taifa,Uhuru na CCM Kirumba pale Mwanza.
HISTORIA
Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi ulijengwa mwaka 1988 wakati wa utawala wa Chama Kimoja chini ya Uongozi wa Rais wa Pili wa Tanzania Mh. Ally Hassan Mwinyi.Historia inasema ujenzi wa uwanja huo ulitokana na Wananchi kuchangia nguvu zao kiihari na hata kilazima mpaka Uwanja ulipokamilika kwa ahadi kwamba uwanja huo ni wa kisasa na itakua chanzo kikubwa cha mapato kwa Mkoa japokua sina uhakika kama lengo hilo limetimia ila nijuavyo sasa CCM wanapata mapato kwa kila shughuli inayofanyika hapo.
Uwanja huo upo katikati ya mji wa Tabora, Mji unaosifika kua na Utajiri wa Wachezaji waliowahi kuwika akiwemo Idd Moshi na haruna Moshi "Boban"
Polisi na Rhino Rangers za Tabora zinazoshiriki ligi ya daraja la kwanza Taifa zinautumia uwanja huo kwa sasa ambapo tabora haina timu inayoshiriki ligi kuu ya Vodacom.
Ally Hassan Mwinyi ni kati ya Viwanja vingi vilivyotelekezwa hapa Tanzania na hii inatokana na vyama vya mikoa kushindwa kutengeneza program za mikoa husika katika kuendeleza soka.
Miwani yangu pana itaendelea kuvumbua yote yasiyoonekana mpaka kutumia Big lens kama yangu kuyasema.
Ukiwa kama Mpenda soka Unadhani nini kinapaswa kufanyika katika viwanja hivi?
,,,,,,,,,,,,,"""" Merry Christmass kwenu Wapenda Soka"""""",,,,,,,,,,
Asante kwa Abel Chimwejo wa wapenda Soka Group kwa kunisaidia kuzipata picha za uwanja huo kwasasa.
Tuonane wakati mwingine na kwa maoni tuwasiliane
wapendasoka@gmail.com au nicheki hewani 0715 12 72 72
sikuwahi kubahatika kukiona hiki kiwanja nilibahatika kuona viwanja vichache sana vya mikoani the like of.tanga,mbeya,morogoro,dodoma and mwanza kiukweli katika viwanja vyote ukitoa uwanja wa mwanzxa huu wa tabora ni moja ya pitvh nzuri kuwai kuiona katika macho yangu ila tu matunzo ndo yanauwa hivi viwanja uwangalie sokoine umekuwa kama jangwa hauna matunzo hata kidogo angalia huu uwanja naamini hauna matunzo mazuri ndo mana uko ivi ila ungekuwa unatunzwa vizuri na kupewa uangalizi basi vilabu vyetu vuingeutumia huu
ReplyDeleteBab tatizo mmiliki wa Viwanja hivi ni nani?
ReplyDeleteKlabu zetu hazina viwanja na viwanja vilivyopo ni vya hawa watawala
ila najua huu uwanja ungekua Hapa Dar ungekarabatiwa
Nikiangalia uwanja huu hua natamani kulia.Ninachokumbuka tangu sherehe za kuzima mwenge mkoani Tabora 1990 ujenzi na uendelezaji wake ulikoma na kuufanya uanze kutumika hali ukiwa bado haujakamilika na kupelekea kua kama gofu.
ReplyDelete