HATUJAJENGA ZAIDI YA MSINGI ALIOTUACHIA MAXIMO
Tarehe 29/6/2006 Tanzania ilishtuka usingizini katika soka la ueledi na kisasa.
Hiyo ndiyo tarehe aliyoajiriwa kocha kutoka Brazil,Marcio Maximo ambaye kila Mtanzania alimpenda.akaandikwa mpaka kwenye daladala.
Nataka tukumbuke Maximo alitukuta na hali gani.Tukumbuke siku ile anaoneshwa uwanja wa Karume ukiwa na udongo mwekundu kwamba ndipo timu ya taifa itakapofanyia mazoezi.kiukweli alitukuta hoi.
Aliikuta Stars ya kina Juma Kaseja,Mecky Maxime,Victor Costa,Chuji,Henry,Nditi, Mrwanda nk wakiwa na jezi za njano.
Kabla hajafika hapa alisoma mahali juu ya soka letu na siasa zake na alipofika akaomba jezi zetu zibadilishwe na zisiwe za njano wala nyekundu.
Tukajazana shamba la bibi pale (uwanja wa uhuru) tukamtazama Maximo na Stars yake ya kwanza akiwakabili Burkina faso.
Mwaikimba na Nizar Khalfan wakampa mbrazil huyo ushindi wa kwanza wa mabao 2-1 ukiwa ni mwanzo mzuri,kila mtu akaipenda Stars,tukaitungia nyimbo na tukaamini sasa tunatoka.
Maximo kama walivo makocha wengi wa kigeni wanaokuja hapa,ni mtu mwenye akili sana alishatusoma akagundua hatuna hata msingi wa soka na kweli,kama timu ya taifa ipo kama timu ya ndondo katika karne ya 21 basi tulikua nchi ya ajabu sana.
Tukaamini tumepata mtu wa kuongoza mapinduzi.
Mpenda soka siku zote hapendi kufungwa,anataka ushindi tu ndio kawaida ya soka hiyo. Hata sisi ambao tulikua nafasi ya 167 kwa viwango vya FIFA,tulitaka tuwafunge Senegal,tena pale pale kwao Dakar.
Kwa kulitambua hilo,Maximo akaanza kwa kutengeneza ngome imara ili walau kupunguza idadi ya magoli huku akijaribu kutujengea msingi wa soka alifanya hivo kwa kujua ushindi katika soka una misingi na njia zake,hauji tu kama ndoto.
Alitamka mwenyewe kwamba,"sikuja kuleta makombe,nimekuja kujenga msingi". Kauli ya ukweli kabisa ambayo inamweka huru. Tatizo letu sisi ni kutaka tuezeke kabla hata ya msingi.
Moja kati ya misingi ya soka ni nidhamu, hakuna ushindi bila nidhamu,hakuna uzalendo bila nidhamu hasa unapocheza timu ya taifa.
Hawa makocha wanaojua taaluma zao huwa ni wakweli na wanasimamia falsafa zao ndiyo maana Sledejovic Milutin Micho akiwa kocha wa Yanga wakati huo alipomwadhibu Hamis Yusuph kwa matatizo ya nidhamu,Maximo alimwondoa Taifa Stars.
Alimwondoa baada ya kuwasiliana na Micho na kuthibitishiwa matatizo ya beki huyo lakini sisi Watanzania hatukutaka kuwaelewa makocha wetu sisi tulichotaka ni kumwona Hamis uwanjani tu basi,pasipo kutaka kujua anahitaji nini ili kuwa uwanjani.
Maximo alijitahidi kujenga msingi kama alivotuahidi japo alipata upinzani kidogo kutoka kwa Watanzania kwa kuwaletea Amir Maftah kutoka Mtibwa,Tegete na Kigi kutoka Makongo akapata nafuu tu baada ya wachezaji hao kusajiliwa na Yanga si unajua tena Simba na Yanga ndiyo wafalme wa soka hapa Tanzania na kila wanachogusa kinapata thamani?
Maisha yakaendelea,tukavuka milima na mabonde,kufungwa magoli matano,kushiriki CHAN nk.
Tukafika mahali watu wakahisi Maximo amewachosha,sababu kubwa ikawa ni wachezaji wao vipenzi,Juma Kaseja,Athuman Idd,Haruna Moshi na Amir Maftah ambao Maximo waliwatosa kwa sababu ya nidhamu, kumbuka ndio tunajenga msingi,hatutafuti kombe la Afrika. Sisi hatukukubali, tukataka tu vipenzi vyetu hivyo viwemo kwenye timu yetu.
Maximo akatuuliza swali moja,"Nilipokuja hapa niliwakuta hao wachezaji wenu,je mlikua mnacheza kombe la dunia na sasa hamchezi kwa sababu hawapo?" tukadhani ametutukana.
Tukafanya uswahili wote kuhakikisha Maximo anaondoka ili sisi tubaki na kina boban,tukasema yote. Nakumbuka katika gazeti la Raia Mwema toleo la 113 Desemba 23,2009 mwandishi alikua analinganisha rekodi za Taifa Stars ya Maximo na za Sunday Kayuni matusi yaliyoje na ukosefu wa fadhila!
Hatimaye siku ya siku ikafika,Maximo akamaliza mkataba wake akaondoka zake,lakini akatuachia msingi kama alivotuahidi yani alichokuja kukifanya akawa amekikamilisha akatuacha walau tunajielewa,tunavaa jezi za timu yetu,wachezaji wanajivunia kuichezea timu ya Taifa, wanajiamini,kwa ufupi tunaeleweka kidogo ndiyo maana ya msingi.
Lakini najaribu kufikiria kama baada ya msingi tungeendelea kua na Maximo ingekuaje? Kwani tangu aondoke tumepiga hatua ngapi?
Kipa ni Kaseja ambaye mimi sidhani kama ni mzuri kwa sasa kulinganisha na Ivo Mapunda ambaye Wakenya wanatamani angekua raia wa huko. Haruna Moshi alishatutia aibu na kimoyomoyo tukamwelewa Maximo hata Chuji alipopatwa na tuhuma za kutumia dawa za kulevya,tulimkumbuka Maximo kimoyomoyo.
Yanga walipomfukuza Maftah kwa kosa la kumbwatukia kiongozi,napo tulimkumbuka Maximo.
Alikuja Jan Paulsen hapa,akatumia msingi wa Maximo kutwaa kombe la CECAFA SENIOR CHALENGE kisha baada ya hapo akatupigisha hatua za kinyumenyume pamoja na yote nae hakusita kutuambia ukweli.
Hamkumbuki alipomwacha Samatta katika kikosi chake kwa madai kuwa siyo mzalendo? Sisi tukaja juu tukamwona anatuzingua tukamfanyia figisu figisu mzee wa watu akaondoka zake!
Hebu tujirudi tumkumbuke Maximo aliyetuachia ushauri murua.
30% ya Stars itokane na wachezaji wa kulipwa.
50% itokane na U-20
40% ya U-20 itoke U-17.
U-17 itokane na clubs,UMISSETA na Academies.
Imeandikwa na Richard Leonce ChardBoy
0658399341
Hiyo ndiyo tarehe aliyoajiriwa kocha kutoka Brazil,Marcio Maximo ambaye kila Mtanzania alimpenda.akaandikwa mpaka kwenye daladala.
Nataka tukumbuke Maximo alitukuta na hali gani.Tukumbuke siku ile anaoneshwa uwanja wa Karume ukiwa na udongo mwekundu kwamba ndipo timu ya taifa itakapofanyia mazoezi.kiukweli alitukuta hoi.
Aliikuta Stars ya kina Juma Kaseja,Mecky Maxime,Victor Costa,Chuji,Henry,Nditi,
Kabla hajafika hapa alisoma mahali juu ya soka letu na siasa zake na alipofika akaomba jezi zetu zibadilishwe na zisiwe za njano wala nyekundu.
Tukajazana shamba la bibi pale (uwanja wa uhuru) tukamtazama Maximo na Stars yake ya kwanza akiwakabili Burkina faso.
Mwaikimba na Nizar Khalfan wakampa mbrazil huyo ushindi wa kwanza wa mabao 2-1 ukiwa ni mwanzo mzuri,kila mtu akaipenda Stars,tukaitungia nyimbo na tukaamini sasa tunatoka.
Maximo kama walivo makocha wengi wa kigeni wanaokuja hapa,ni mtu mwenye akili sana alishatusoma akagundua hatuna hata msingi wa soka na kweli,kama timu ya taifa ipo kama timu ya ndondo katika karne ya 21 basi tulikua nchi ya ajabu sana.
Tukaamini tumepata mtu wa kuongoza mapinduzi.
Mpenda soka siku zote hapendi kufungwa,anataka ushindi tu ndio kawaida ya soka hiyo. Hata sisi ambao tulikua nafasi ya 167 kwa viwango vya FIFA,tulitaka tuwafunge Senegal,tena pale pale kwao Dakar.
Alitamka mwenyewe kwamba,"sikuja kuleta makombe,nimekuja kujenga msingi". Kauli ya ukweli kabisa ambayo inamweka huru. Tatizo letu sisi ni kutaka tuezeke kabla hata ya msingi.
Moja kati ya misingi ya soka ni nidhamu, hakuna ushindi bila nidhamu,hakuna uzalendo bila nidhamu hasa unapocheza timu ya taifa.
Hawa makocha wanaojua taaluma zao huwa ni wakweli na wanasimamia falsafa zao ndiyo maana Sledejovic Milutin Micho akiwa kocha wa Yanga wakati huo alipomwadhibu Hamis Yusuph kwa matatizo ya nidhamu,Maximo alimwondoa Taifa Stars.
Alimwondoa baada ya kuwasiliana na Micho na kuthibitishiwa matatizo ya beki huyo lakini sisi Watanzania hatukutaka kuwaelewa makocha wetu sisi tulichotaka ni kumwona Hamis uwanjani tu basi,pasipo kutaka kujua anahitaji nini ili kuwa uwanjani.
Maximo alijitahidi kujenga msingi kama alivotuahidi japo alipata upinzani kidogo kutoka kwa Watanzania kwa kuwaletea Amir Maftah kutoka Mtibwa,Tegete na Kigi kutoka Makongo akapata nafuu tu baada ya wachezaji hao kusajiliwa na Yanga si unajua tena Simba na Yanga ndiyo wafalme wa soka hapa Tanzania na kila wanachogusa kinapata thamani?
Maisha yakaendelea,tukavuka milima na mabonde,kufungwa magoli matano,kushiriki CHAN nk.
Tukafika mahali watu wakahisi Maximo amewachosha,sababu kubwa ikawa ni wachezaji wao vipenzi,Juma Kaseja,Athuman Idd,Haruna Moshi na Amir Maftah ambao Maximo waliwatosa kwa sababu ya nidhamu, kumbuka ndio tunajenga msingi,hatutafuti kombe la Afrika. Sisi hatukukubali, tukataka tu vipenzi vyetu hivyo viwemo kwenye timu yetu.
Maximo akatuuliza swali moja,"Nilipokuja hapa niliwakuta hao wachezaji wenu,je mlikua mnacheza kombe la dunia na sasa hamchezi kwa sababu hawapo?" tukadhani ametutukana.
Tukafanya uswahili wote kuhakikisha Maximo anaondoka ili sisi tubaki na kina boban,tukasema yote. Nakumbuka katika gazeti la Raia Mwema toleo la 113 Desemba 23,2009 mwandishi alikua analinganisha rekodi za Taifa Stars ya Maximo na za Sunday Kayuni matusi yaliyoje na ukosefu wa fadhila!
Hatimaye siku ya siku ikafika,Maximo akamaliza mkataba wake akaondoka zake,lakini akatuachia msingi kama alivotuahidi yani alichokuja kukifanya akawa amekikamilisha akatuacha walau tunajielewa,tunavaa jezi za timu yetu,wachezaji wanajivunia kuichezea timu ya Taifa, wanajiamini,kwa ufupi tunaeleweka kidogo ndiyo maana ya msingi.
Lakini najaribu kufikiria kama baada ya msingi tungeendelea kua na Maximo ingekuaje? Kwani tangu aondoke tumepiga hatua ngapi?
Kipa ni Kaseja ambaye mimi sidhani kama ni mzuri kwa sasa kulinganisha na Ivo Mapunda ambaye Wakenya wanatamani angekua raia wa huko. Haruna Moshi alishatutia aibu na kimoyomoyo tukamwelewa Maximo hata Chuji alipopatwa na tuhuma za kutumia dawa za kulevya,tulimkumbuka Maximo kimoyomoyo.
Yanga walipomfukuza Maftah kwa kosa la kumbwatukia kiongozi,napo tulimkumbuka Maximo.
Alikuja Jan Paulsen hapa,akatumia msingi wa Maximo kutwaa kombe la CECAFA SENIOR CHALENGE kisha baada ya hapo akatupigisha hatua za kinyumenyume pamoja na yote nae hakusita kutuambia ukweli.
Hamkumbuki alipomwacha Samatta katika kikosi chake kwa madai kuwa siyo mzalendo? Sisi tukaja juu tukamwona anatuzingua tukamfanyia figisu figisu mzee wa watu akaondoka zake!
Hebu tujirudi tumkumbuke Maximo aliyetuachia ushauri murua.
30% ya Stars itokane na wachezaji wa kulipwa.
50% itokane na U-20
40% ya U-20 itoke U-17.
U-17 itokane na clubs,UMISSETA na Academies.
Imeandikwa na Richard Leonce ChardBoy
0658399341
maximo utabaki kuwa wimbo ulioimbwa kuitakia tanzania mema ila watu wake hawakujitakia mema.
ReplyDeletealitupenda, alitaka tuwe wenye mafanikio, ila viongozi wa tff walikuwa hawataki walimuangusha hadi Mh Rais alijitoa kutaka kuona mafanikio