Peter Ndlovu MAHUTUTI apata ajali MBAYA

 
Peter Ndlovu kwenye uzi ya Sundowns

Mchezaji aliyewahi kucheza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza Peter Ndlovu, jana Jumapili alikimbizwa Hospitali jijini Bulawayo Zimbabwe baada ya kupata ajali mbaya iliyotaka kuchukua uhai wake, ajali hiyo imemsababishia majeraha makubwa na kusababisha kifo cha kaka yake mmoja aliyekuwamo ndani ya gari hilo.

Gari aina ya BMW lililokuwa linaendeshwa na Adam Ndlovu likiwa nje ya barabara


Peter Ndlovu, 39, amewahi kuzichezea timu kadhaa nchini Uingereza  ikiwemo Coventry , timu ambayo alianza kuichezea na kuing’aza nyota yake, pia aliwahi kuzichezea timu za Birmingham, Huddersfield  na Sheffield United, kabla ya kurudi  na kuendelea kucheza soka kwenye klabu za Afrika mnamo mwaka 2004.
Ajali hiyo iliyosababisha kifo cha kaka yake ilitokea usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili. Mshambuliaji huyu mwenye uwezo wa juu aliachana na timu yake ya nyumbani  Highlanders na kuamua kujiunga na timu ya Coventry mnamo mwaka 1991 na kuichezea timu hiyo ya barabara ya Highfield mpaka mwaka 1997.
 Pembeni ya Barabara ilipougonga mti
Taarifa iliyotolewa na klab yake ya zamani ambayo kwa sasa ipo kwenye npower League One, inaeleza: 'Coventry City Football Club imesikitishwa juu ya habari mbaya ya barabarani iliyotokea nchini Zimbabwe, ajali inayomuweka kwenye hali mbaya mshambuliaji wetu wa zamani Peter Ndlovu, ajali imepelekea kuchukua uhai  wa kaka yake aitwae Adam. 
Peter Ndlovu kushoto alipokuwa anaichezea Coventry na kulia alipokuwa anaichezea Birmigham
 
'Imeelezwa pia ndugu hao wawili walikuwa wanatoka kuangalia mechi ya ugenini kati ya timu ya Chicken Inn FC dhidi ya timu yao ya nyumbani, na wakiwa njiani wanarudi tairi la gari ya Ndlovu lilipasuka nakusababisha gari kupoteza uelekeo eneo ambalo lipo umbali wa kilometa 20 toka yalipo Maporomoko ya Victoria.
Adam Ndlovu: Aliyewahi kuichezea Zimbabwe, amefariki katika ajali hiyo.
Ndlovu aliichezea Birmigham mechi 137 na kufanikiwa kufunga jumla ya magoli 28 kwenye mashindanio yote. Alijiunga kwa mkopo na timu ya Huddersfield kwenye kipindi cha baridi msimu wa 2000-01, akiifungia timu hiyo magoli manne kwenye michezo sita, alihama Birmingham mnamo Febuari 2001 na kujiunga na Sheffield United kama mchezaji huru.
Alicheza jumla ya mechi 154 kwenye klabu ya Bramall Lane, na kuweza kufunga jumla ya magoli 29, na kuachana nayo mnamo Julai 2004 aliporudi kucheza kwenye klabu za Afrika.

1 comment:

  1. duuuh mungu mkubwa na wakushukuriwa umu ametoka mtu na mzima daaah hatariii

    ReplyDelete

Powered by Blogger.