UEFA CHAMPIONS LIGI: Ni Patashika Juventus v Chelsea

 
USHINDI MUHIMU kwa kila Timu, au BALAA
MECHI: Novemba 20 UWANJA: Juventus Arena, Turin, Italy
Mabingwa wa Ulaya, Chelsea, wanaikwaa Juventus, Mabingwa wa Italy, na kila mmoja anataka ushindi ili ajihakikishie anatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI lakini hii ni Mechi isiyotabirika ukizingatia Mwezi Septemba, ndani ya Stamford Bridge, Chelsea waliongoza Bao 2-0, kwa Bao za Oscar, lakini Juve wakazinduka na kusawazisha kwa Mabao ya Arturo Vidal na Fabio Quagliarella na kutoka 2-2.
 
KUNDI E MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Shakhtar Donetsk Pointi 7
2 Chelsea 7
3 Juventus 6
4 Nordsjaelland 1 [NJE]
 
FAHAMU: Timu mbili za juu toka kila Kundi zinaingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na Timu itakayomaliza nafasi ya 3 itaingizwa EUROPA LIGI.
 
Ikiwa Chelsea hawatafungwa na Juventus ni wazi watafuzu kwani Mechi yao ya mwisho ni nyumbani Stamford Bridge dhidi ya Nordsjaelland ambayo imeshatupwa nje ya Mashindano na ambayo Chelsea waliibonda Bao 4-0 huko kwao Denmark.
Chelsea wataingia kwenye Mechi hii bila ya nguzo yao kubwa, Nahodha wao John Terry, ambae ni majeruhi lakini Mabingwa hawa wa Ulaya nguzo yao kubwa zaidi ni Mashambulizi wakitegemea kasi na ushirikiano wa kina Ramires, Eden Hazard, Oscar, Juan Mata kumlisha Straika wao Fernando Torres.
Juve, wakiongozwa na Mkongwe Andrei Pirlo kwenye Kiungo na ambao walitoka sare Mechi zao zote 3 za kwanza za Kundi hili na kuzinduka tu katika Mechi ya 4 walipowaponda vibonde Nordsjaelland Bao 4-0, wana Wachezaji wengine hatari kama vile Kiungo Claudio Marchisio [Pichani], Mirko Vucinic, Arturo Vidal na Fabio Quagliarella.
Hawa wanatisha hasa ukizingatia Chelsea, chini ya Kocha Roberto Mancini, ina Difensi ‘nyanya’ ambayo imevujisha Mabao 17 katika Mechi zao 8 zilizopita.
Katika Mechi za Ligi zao za Wikiendi hii iliyopita, Chelsea walichapwa 2-1 na WBA na Juventus kuambua sare ya 0-0 walipocheza na Lazio bila ya kuwa na nguzo yao kubwa Andrei Pirlo ambae alikuwa kifungoni.
Juve, ambao wapo chini ya Kocha Angelo Alessio kwa vile Kocha wao Antonio Conte yuko kifungoni, wameshatamka hii ni ‘Mechi yao ya Mwaka.’
Hakika ni patashika.

No comments

Powered by Blogger.