MAN UNITED NA SPURS ZAAMBULIA VIPIGO EUROPA LEAGUE
Hatua ya 16 bora ya michuano ya Europa League ilianza usiku wa jana kwa timu zote 16 kujitupa viwanjani kusaka ushindi wake wa kwanza katika mechi mbili za hatua hii.
Manchester United wakisafiri ugenini kuwavaa Liverpool katika dimba la Anfield na wenyeji Liverpool waliibuka na ushindi wa bao 2-0 katika mchezo ambao uliotawaliwa na Liverpool huku United wakipoteana hasa Kipindi cha kwanza hali iliyopelekea wasiweze kupata hata shuti moja lililolenga lango kwa kipindi hicho cha kwanza.
Liverpool walipata magoli yao kupitia kwa Daniel Sturadge kwa njia ya penati na Roberto Firminho aliyetumia uzembe wa Michael Carrick ambaye aliingia kucheza beki wa kati akichukua nafasi ya Rashford.

Kuangalia Magoli ya mechi zote ingia hapa
EUROPA LEAGUE: ANGALIA MAGOLI YA MECHI ZOTE ZA JANA HAPA
Huko Ujerumani wenyeji Borussia Dortmund waliilaza Tottenham Hotspurs bao 3-0 katika mechi nyingine hiyo jana wenyeji wakipata magoli kupitia kwa Pierre Emenick Obemeyang na Marco Reus aliyefunga bao mbili.
Valencia wakiwa ugenini walifumuliwa bao 1-0 ugenini wakifungwa na Atletico Bilbao wakati Mabingwa watetezi Sevilla walilazimishwa Sare ya bila kufungana na FC Basel.
Mechi za marudiano zitachezwa Alhamisi Ijayo

MATOKEO YOTE YA MECHI ZA JANA EUROPA LEAGUE
- Fenerbahce 1-0 Braga
- Borussia Dortmund 3-0 Tottenham Hotspur
- FC Basel 0-0 Sevilla FC
- Shakhtar Donetsk 3-1 Anderlecht
- Villarreal 2-0 Bayer Leverkusen
- Athletic Bilbao 1-0 Valencia
- Liverpool 2-0 Manchester United
- Sparta Prague 1-1 Lazio

No comments