LICHA YA USHINDI MNONO MASHABIKI ARSENAL WAMTAKA WENGER AJIUZULU

Katika hali isiyotegemewa mashabiki wa Arsenal jana walibeba Bango la kumtaka kocha wao Arsene Wenger ajiuzulu nafasi hiyo katika mechi ya kombe la FA dhidi ya Hull city katika dimba La KC.





Arsenal iliibuka na ushindi mkubwa wa bao 4-0 katika mechi hiyo ya marudiano baada ya kushindwa kupata mshindi katika mechi ya awali katika dimba La Emirates Jijini London.

Magoli ya Arsenal hiyo jana yalifungwa na Oliver Giroud mabao mawili na Theo Walcott naye akifunga mabao mawili katika mechi ambayo Per Metesacker,Gabriel Paulista na Aaron Ramsey wote wakitolewa kwa kupata majeraha.

Kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger alikataa kabisa kuzungumzia hali iliyojitokeza na kusema ameshawazoea yeye anahakikisha timu inapata ushindi na ndo alichokifanya jana.

No comments

Powered by Blogger.