CHELSEA MAMBO YALE YALE , EVERTON YAIADABISHA NEWCASTLE
Mambo yanazidi kuwaendea Kombo mabingwa watetezi wa Ligi kuu nchini England Chelsea baada ya jana usiku kulazimishwa sare ya bila kufungana na timu iliyopanda daraja ya Watford.
Chelsea wanaokamata nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi kuu ilisafiri kuwakabili Watford wakitaka japo kujikwamua na matokeo mabaya msimu huu lakini waliambulia sare hiyo ambayo inawapandisha Watford katika nafasi ya 9.

EPL: ANGALIA MATOKEO YA MECHI ZA LIGI KUU UINGEREZA (VIDEO)
Angalia magoli yote kwa mechi za jana hapa
Katika mechi nyingine pale Goodson Park wenyeji Everton walikua nyumbani kuwakabili Newcastle walio katika hatari ya kushuka daraja.
Everton waliiadabisha Newcastle kwa kuifunga bao 3-0 huku Rose Barkley akifunga mabao mawili yakiwa yote ni ya Penati huku Aaron Lenon akitangulia kwa kufunga bao la kwanza.
Kwa matokeo hayo Everton wanafikisha pointi 32 katika nafasi ya 11 huku Newcastle United wakizidi kujichimbia shimo la kushuka daraja wakiwa katika nafasi ya 18 na pointi 21.
No comments