RASMI : MAN UNITED YAPELEKA OFA YA KUMSAJILI SERGIO RAMOS



Baada ya kutawaliwa na tetesi nyingi katika mitandao mbalimbali zikimuhusisha beki wa Kimataifa wa Spain na klabu ya Real Madrid kutaka kujiunga na Manchester United hatimaye mabingwa hao wa Kihistoria wa ligi kuu ya England wamepeleka ofa rasmi ya kutaka kumsajili beki huyo anayecheza nafasi ya beki wa kati au pembeni na hata kiungo mkabaji.

Manchester United wamepeleka ofa ya paundi milioni 28.6 ili kumnasa beki huyo anayesifika kwa uhamasishaji na kufunga magoli ya vichwa.

Mchezaji huyo mwenye miaka 29 alinukuliwa kuwa anataka kuihama Real Madrid baada ya kushindwa kumpa mkataba mpya baada ya ule wa awali kubaki mwaka mmoja uishe.

Ramos ameichezea Real Madrid michezo 445 tangu alipojiunga na wababe hao wa Soka la ulaya akitokea Sevilla mwaka 2005.

Katika nafasi ambazo kocha wa Man United atataka kuzijaza msimu huu ni beki wa kati baada ya msimu uliopita kuambulia nafasi ya nne huku wachezaji waliocheza nafasi hizo kutoonyesha makali yaliyotarajiwa

No comments

Powered by Blogger.