MFAHAMU BEKI SHUJAA ALIYEDAKA PENATI MBILI LIGI YA MABINGWA ULAYA.
COSMIN MOTI ni jina ambalo halitasahaulika katika vinywa vya Wapenda Soka nchini Bulgaria ambako anacheza soka la kulipwa lakini pia nchini kwao Romania ambako amezaliwa kijana huyu mrefu mwenye umri wa miaka 29.
Cosmin Moti ni beki wa kimataifa wa Romania anayekipiga katika klabu ya PFC Ludogorets Razgrad ya Bulgaria aliyezaliwa tarehe 3 Desemba mwaka 1984 nchini Romania.
Huyu ndo shujaa ambaye usiku wa Jumatano wiki hii aliweza kuipeleka timu yake katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya ambapo sasa wamepangwa katika kundi B pamoja na mabingwa watetezi Real Madrid, FC Basel na Liverpool.
Ulikua mchezo wa pili wa hatua ya mtoano kati ya Ludogorets ikiikaribisha Timu toka nchini Romania Steau Bucharest ambako Cosmin ndo alikozaliwa.
Katika mchezo huo Cosmin akicheza nafasi ya mlinzi alijikuta akikabidhiwa jukumu la kuwa kipa wa Ludogorets baada ya kipa wa timu hiyo Vladislav Stoyanov kutolewa nje kwa kadi nyekundu huku Wakiwa wameshakamilisha idadi ya wachezaji watatu wa akiba.
Baada ya kutoka na ushindi wa bao 1-0 Ludogorets walikua wakilingana matokeo ya jumla na Steau yani 1-1 baada ya Steau kushinda goli 1-0 katika mechi ya awali huko Romania.
Cosmin akipiga penati ya kwanza na kuokoa nyingine mbili aliiwezesha Ludogorets kutinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo sasa watajihakikishia dola milion11 kwa kuingia tu hatua hii ya makundi haijalishi kama watashinda mchezo wowote au watafungwa.
Huyu ndo COSMIN MOTI subiri kuona shughuli yake atakapopambana na Real Madrid,Liverpool au FC Basel.
~ Edo Daniel Chibo
No comments