UPAMBE WA KAIJAGE KWENYE HARUSI YA KISPANYOLA,ZURICH(part 1) ...... Nashukuru mungu kwa kunipa nafasi ya kua mmoja wa wapambe kwenye harusi hii ya kispanyola huko zurich,kwenye harusi kuna watu wengi mashuhuri lakini bibi na bwana harusi ndo mabosi wa sherehe.. Hata ukiwa maarufu kiasi gani.. Jina la bibi na bwana harusi vitatawala mdomoni mwa mc..... Bibi na bwana harusi watakua bora kuliko watu wote harusini....Nimehudhuria harusi nyingi lakini hii naisubiri kwa hamu...harusi hii ni ya ajabu ..harusi hii inanikumbusha kitabu kimoja pendwa kiitwacho "three suitors one husband" ... Kwenye hii harusi kuna madume watatu lakini anatakiwa mume mmoja tu.... Cha ajabu midume yote inajiona inastahili kumchukua mwanamwali.....pia mwanamwali anaona anastahili kuolewa na mwanaume yeyote kati ya hao watatu ...hama kweli hii ni harusi ya dunia.... Madume hayo yametoka sehemu tofauti japo yote yamelowea spain.. Dume la kwanza kutoka Argentina mloezi wa spai
n,la pili kutoka portugal pia mloezi wa spain na Dume la mwisho ni kutoka spain... Kila Bwana harusi amekuja na wapambe wake.... Na kila mpambe anataka dume lake ndo lichukue mwanamwali..... Ikambidi mzazi wa bibi harusi Aitwaye seif blatter mkazi wa zurich atumie busara na hekima.....Dunia nzima ikawa na shahuku ya kusikiliza nini mzazi wa bibi harusi atasema kuhusiana na ndoa ya binti yake.. Mzazi huyo wa bibi harusi akaamua kuunda kundi dogo la watu ambao wanajua sifa za bwana harusi bora... Wachunguze kisha wapige kura yupi anafaa kuondoka na mwanamwali..... Uamuz huo wa busara kabisa kuchukuliwa na wazazi wa upande wa bibi harusi kwa pamoja (fifa)..... Kundi hilo au kamati hiyo itaangalia nini kila bwana harusi alifanya kwa mwaka mmoja ulopita ili astahili kuitwa mwanaueme bora kuliko wenzake..... Kuna njia nyingi za kujua wewe ni mwanume au mume bora....Lakini cha kustahabisha Wanaume hawa wamefanana kwa vitu vingi sana maumbo,sura pia hata mvuto Lakini pia Bahati ilioje wote wamejikuta ni wasakata kabumbu.... Hyo ndo ikawa sifa kubwa na ya pekee kujua na kuwatofatisha yupi ni bora kati yao... Basi Kamati ikaamua Iegemee katika sifa ya kusakata mpira wa miguu.... Nilivyosikia hvyo nikastaajabu nikisema moyoni ni hekima ya namna gani mungu amewajaria wazazi wa bibi harusi. inafanana na hile ya meshack,shadrak na abednego na pia kidogo kutoka kwa suleiman..... Sasa ikafika zamu ya kamati kuletewa sifa za kila mmoja kuzichambua kabla ya kupiga kura...................... To be continue(itaendelea)...................................................................



2 comments:

Powered by Blogger.