MIWANI PANA YA EDO ~ OLE GUNNAR SOLSKJAER NA NAFASI YA KUMRITHI ALEX FERGUSON (MAN UNITED)

    

     

Ole Gunnar Solskjær mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Norway na Mabingwa wa kihistoria wa England ( Manchester United) amezaliwa Tarehe 26 Februari 1973 (miaka 39)
Ole ametumia maisha yake ya soka miaka mingi akiichezea Man United kama Mshambuliaji na mara chache kama winga.
Kabla ya kujiunga na Man United alizichezea klabu za ligi ya Norway za Clausenengen na Molde  FK ambayo hivi sasa anaifundisha kama kocha na meneja.
Ole Alijiunga na Man United mwaka 1996 kwa uhamisho wa Paund 1.5 million na alikua akijulikana sana kwa jina la utani "Muuaji mwenye sura ya kitoto"
Aliichezea Man united Michezo 366 na kufunga magoli 126 akijulikana kama "Super sub" kwa kipaji alichokua nacho cha kutokea benchi na kufunga magoli muhimu na anakumbukwa zaidi kwa goli la dakika ya mwisho la ushindi katika fainali ya Ligi ya mabingwa wa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.



                                  ANA HISTORIA GANI KATIKA UKOCHA
Baada ya kushindwa kupona maumivu ya goti yaliyokua yakimsumbua mara kwa mara,Mwaka 2007 Ole alitangaza kustaafu soka na kubaki klabuni Manchester katika kazi ya ukufunzi wa soka
na mwaka 2008 Ole akawa kocha wa Timu ya wachezaji wa akiba wa Man United (hii ni kama nafasi ya Alex Ferguson) kwani wachezaji wengi walio akiba ni wale walio majeruhi ya kikosi cha kwanza na ambao hawapati nafasi ktk kikosi cha kwanza katika kikosi cha SAF.


Mwaka 2011 Ole alirudi Norway kuifundisha timu yake iliyomtoa ya Molde FK ambapo aliiongoza kutwaa ubingwa wa ligi kwa mara ya kwanza ktk historia ya club hiyo na mwaka huu 2012 ameshachukua ubingwa kwa mara ya pili mfululizo ndani ya miaka miwili.
Ole amesaini mkataba wa miaka minne kuifundisha Molde FK na katika mechi yake ya kwanza ktk ligi ya Norway akiwa kama
kocha wa Molde alijikuta akitandikwa 3-0 toka kwa timu iliyopanda daraja Sarpsborg 08.
Mechi ya kwanza akiwa kama Kocha wa Molde ktk uwanja wa nyumbani aliambulia droo ya 2-2 dhidi ya kinara wa ligi Tromso huku goli la kwanza kwake ktk klabu hiyo likifungwa na Msenegali Papa Pate Diouf.
Mwezi Oktoba akiiongoza Molde kutwaa ubingwa wa kwanza ktk historia ya klabu hiyo  huku ukiwa ni mwaka wa 100 tangu kuanzishwa Molde FK.





   Tarehe 18 May 2012 Ole alipata ruhusa kutoka ktk klabu yake ya Molde kufanya mazungumzo na na Aston Villa baada ya kumfukua
kocha wao Alex McLeish japokua Ole aliamua kubaki na timu yake Molde kuepusha kuisumbua familia yake amabyo ilishaeka makazi Norway.
November 11,2012 imekua tarehe ya kihistoria baada ya kuiongoza Molde kushinda ubingwa wa Norway kwa mara ya 2 mfulizo kwa kuwafunga Honefoss 1-0.

                            
                                    REKODI KAMA KOCHA
Ameanza kuifundisha Molde FK November 9,2011 na amefanikiwa kuweka rekodi zifatazo:
     Amefundisha michezo 64
     Akishinda 40 kati ya hiyo
     Amedroo 11
     Amepoteza 13
     Timu imefunga magoli 135
     Na imefunga magoli 70
Huku rekodi ikimweka na Ushindi wa 62.5%

                               

                                 JE SOLSKJAER ANAWEZA KUMRITHI FERGUSON?

Beki wa zamani wa Man United Ronny Johnsen anaamini Ole ndo atakua mrithi wa Ferguson Old Trafford
Ronny alinukuliwa akisema anaamini Ole baada ya kuwa kocha wa timu ya wachezaji wa akiba wa United baadae kurudi Norway na kuiwezesha Molde FK kuchukua ubingwa kwa mara ya kwanza ktk historia ya club hiyo
Pamoja na  uvumi ulioenea kumuhusisha Ole na nafasi ya meneja wa Aston
Villa na hizi taarifa za sasa zilizoenea zikimuhusisha Ole na nafasi ya u meneja Blackburn Rovers na Bolton timu za daraja la kwanza anaamini kuwa Ole kashafanya vizuri sana
kama kocha kwa kipindi kifupi na akifanya vizuri pia ktk Europa itazidi kumpa sifa za kuweza kumrithi SAF.
    Wadau wengi wa soka wanayazungumzia majina makubwa ktk kuirithi nafasi ya Sir alex Ferguson wakiwemo pia Pep Guadiola(kocha wa dhamani wa Barcelona), Jose Mourinho,Moyes n.k lakini mimi naamini Solskjaer anastahili nafasi ya kumrithi Sir Ferguson:

  Kwanza huyu ni mchezaji ambaye alikua akijulikana kama supa sub na hii ilitokana na uwezo aliokua nao ktk kubadili matokeo ya mchezo alipokua akitokea bench wakati akicheza United Ikumbukwe si wachezaji wote wanaoweza kuanza bench na kurekebisha mapungufu waingiapo hivyo elimu yake ya ukocha ilianzia hapo.
  Pili ameweza kukopi njia anazozitumia Sir Ferguson ktk kuibadilisha Molde FK mpaka kupelekea wachambuzi wa mpira kuiita Manchester united ndogo.
  Tatu Ole ameweza kuonyesha uwezo mkubwa wakati akiifundisha Man United kama kocha wa wachezaji wa akiba na hii kumpa nafasi ya kufanya vizuri kama atapewa timu kuifundisha na amelidhihirisha hilo akiwa na Molde
  Nne Makocha wengi maarufu km Guadiola hawakufahamika kabla hawajashika nafasi ya kuzifundisha timu kubwa na hiki pia nakiona kwa Ole.
  Tano Ole ni mchezaji aliyeitumikia United kwa mafanikio makubwa na hii itamfanya kuipenda timu na kuifundisha kwa moyo wake wote.
Ukiacha Ole Gunnar Solskjaer makocha wengine wanaotajwa kumrithi Ferguson ni Pep GUadiola, Jose Mourinho, Jurgen Klopp na Moyes.

 

HUYU NDO OLE GUNNAR SOLSKJAER AMBAE MIMI EDO NAAMINI ANAFAA KUMRITHI SIR FERGUSON

3 comments:

  1. whenever they need a goal they must depend and rely on ole ole ole ole

    ReplyDelete
  2. Anafaa kumrithi bila kipingamizi, na natamani iwe ivyo!

    ReplyDelete
  3. Mi nadhani huyu jamaa atatufaa sana if we can create our classy football palyer the likes of Wazza CR7 Beckham
    Giggs,Scholes and many more why dont we create our own managers to step on the feet of great managers who passed in our club? Busby, Ferg are remarkable in the History of United and world soccer

    ReplyDelete

Powered by Blogger.