EPL: MAN UTD YASHINDA 3, ARSENAL YATULIZWA NYUMBANI, MAN CTY NA LEICESTER VICHEKO (+HIGHLIGHTS)

Manchester United imeibuka na ushindi wa goli 3 kwa 0 dhidi ya Stoke cty. Wakicheza kwa kushambulia lango la timu pinzani na muunganiko wa Martial, Rooney, Mata na Lingard ulitosha kuwachanganya mabeki wa Stoke na kujikuta wako nyuma kwa goli 2 ndani ya dakika 23.


Goli la kwanza la Man utd lilifungwa na Jesse Lingard baada ya kutumia vizuri mpira uliopigwa na beki Bortheick-Jackson  dakika ya 14. Antonio Martial alifunga goli la pili baada ya kumalizia kazi nzuri ya Wayne Rooney. Dakika ya 53 Wayne Rooney alifanikiwa kukamilisha goli la 3 kwa kumalizia mpira uliopigwa na Martial.

Katika michezo mingine Manchester Cty walisafiri hadi kwa wenyeji wao Sunderland na kufanikiwa kuondoka na ushindi wa goli 1 kwa bila goli lililofungwa na mshambuliaji wao hatari Sergio Kun Aguero dakika 16.

Delle Alli alifunga goli moja na Harry Kane alifunga magoli mawili na kuifanya Totenham kuibuka kidedea kwa ushindi wa goli 3 dhidi ya Nowrich, hivyo kupanda hadi nafasi ya 3 na kuishusha Arsenal ambao wametoa sare ya bila kufungana na Southampton.

Vardy aliendelea kuwa mwiba kwa timu pinzani baada ya kufunga mabao 2 dhidi Liverpool na kuisadia timu yake ya Leicester city kuendelea kukaa kileleni kwa kufikisha pointi 50 baada ya kucheza mechi 24. Kwa magoli haya Vardy amefikisha goli 18 na kuongoza orodha ya wafungaji bora katika ligi ya Uingereza.

Matokeo ya Mechi za Leo ni kama ifuatavyo.


Angalia Highlights za mechi za leo hapa

Man Utd 3 - 0 Stoke City


Sunderland 0 - 1 Man City


Nowrich City 0 - 3 Totenham Hotspur


Arsenal 0 - 0 Southampton


Leicester City 2 - 0 Liverpool



West Ham Utd 2 - 0 Aston VIlla

No comments

Powered by Blogger.