WAPENDASOKA FC WAPOTEZA MBELE YA MABABU FC

Mchezo wa kirafiki kati ya Wapendasoka FC dhidi ya Mababu FC uliopigwa jioni ya leo katika kiwanja cha Jakaya Kikwete Youth Park umemalizika kwa Mababu FC kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-2.

Wapendasoka FC itabidi wajilaumu wenyewe kwani kuna wakati waliongoza mchezo huo kwa mabao 2-0 ya Vonso Almeida na Humprey Mrope kabla ya Anatory Gabriel Wa Mababu kuifungia bao timu yake dakika chache kabla ya mapumziko na kufanya timu hizo kwenda kupumzika matokeo yakiwa 2-1.

Kipindi cha pili hakikua kizuri kwa Wapendasoka, kwani Sabry Seif alifanikiwa kuisawazishia Mababu FC kwa shuti kali la karibu na lango.
Sabry Seif aliendelea kuwa nyota wa mchezo baada ya kuandika mabao mengine mawili na kuihakikishia Mababu FC ushindi huo mnono huku yeye mwenyewe akiondoka na mpira wake baada ya kufunga mabao matatu (hat trick)

Hadi mchezo unamalizika, Mababu FC 4-2 Wapendasoka.

Mchezo huo ulikua ni katika muendelezo wa matukio ya Wapendasoka Tanzania kuelekea mwisho wa mwaka ambapo mambo mengi ya kijamii hufanyika ikiwemo kutoa misaada jwa watoto yatima.

Akiongea na tovuti hii baada ya mchezo, Katibu mkuu wa Wapendasoka Richard Leonce aliwashukuru wote walioshiriki kufanikisha mchezo huo na kuongeza kuwa bado kuna mengi wanayotarajia kuyafanya.

"Tulikua na get together kwa wanachama wetu wiki iliyopita, jana tulishiriki kufanya usafi katika hospitali ya Mwananyamala na leo tumecheza mchezo huu. Japo tumepoteza lakini nia yetu ni kuwaweka pamoja vijana na kudumisha undugu wenye tija kwa jamii yetu."
Alisema Richard.
Kikosi cha Mababu Fc
Kikos cha Wapendasoka 

No comments

Powered by Blogger.