UVUMILIVU UMEWASHINDA, EVERTON WAMTUPIA VIRAGO KOEMAN
Klabu ya
Everton imeshindwa kumvumilia kocha wao Ronald Koeman baada ya kumtimua
kufuatia vigigo vya mfululizo wanavyoendelea kuvipata.
Everton imeshinda mechi mbili pekee za ligi
msimu huu ikiwa nafasi ya 18 kwenye msimamo na pia wakiburuza mkia kwenye kundi
E katika michuano ya Europa.
Kipigo cha mabao 5-2 walichokipata jana kutoka
kwa Arsenal na kile cha mabao 2-1 dhidi ya Olympic Lyon kwenye michuano ya
Europa vimechangia kwa kocha huyo raia wa Uholanzi kutupiwa virago hii.
Klabu hiyo imetangaza maamuzi hayo mchana wa leo
baada ya Mwenyekiti wake Bill Kenwright na Mkurugenzi mtendaji Robert Elstone
kuwasili kwenye uwanja wa mazoezi wa mazoezi wa timu hiyo.
Kocha wa timu ya vijana ya miaka 23 David
Unsworth atakaimu nafasi hiyo kwa muda ambapo watasafiri kucheza na Chelsea
katika kombe la ligi keshokutwa Jumatano kabla ya kukutan na Leicester City
Jumapili ijayo.


No comments