SIMBA YAIFATA YANGA 16 BORA KOMBE LA FA


Vinara wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara Wekundu wa Msimbazi Simba wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya  michuano ya kombe la shirikisho la mpira wa miguu nchini maarufu kama Azam Sports Federations Cup(ASFC) baada ya kuifunga timu ya Polisi Dar es Salaam bao 2-0.

Mchezo huo uliochezwa jioni ya leo katika uwanja wa Uhuru jijini ulishuhudia Simba ikipata bao la mapema kabisa likifungwa na Pastory Athanas dakika 4 tu baada ya kuanza mchezo huo pasi kutoka kwa Ibrahim Ajib ikimfikia Shiza Kichuya ambaye aliwahadaa mabeki wa Polisi na kumwacha Pastory mwenyewe ambaye aliuweka mpira kimiani.

Mpaka mapumziko Simba ilikua mbele kwa bao hilo moja licha ya kosakosa nyingi langoni mwa Polisi huku uhodari wa kipa wao Salum Kondo ukiwabeba Polisi mpaka dakika ya 82 pale Mohamed Hussein alipovunja mtego wa Polisi na kuweza kuchomoka na kupiga mpira uliomvuka kipa wa Polisi na kugonga mwamba kisha akauwahi na kuumalizia kuiandikia Simba bao la pili.

Mpaka mwisho wa mchezo Simba waliibuka washindi kwa bao hizo 2-0  na katika mchezo huo kocha wa Simba alifanya mabadiliko ya kuwatoa  Ibrahim Hajib,Mwinyi Kazimoto na Pastory Athnas  huku nafasi zao zikichukuliwa na said Ndemla,Jamal Mnyate na Laudit Mavugo.

 Matokeo mengine ya michezo ya Leo ni

  •  Mbeya Kwanza 1-2 Tanzania prisons (Sokoine,Mbeya),
  • Ruvu shooting 1-2Kiluvya United, (Mabatini Kibaha)
  • Toto African kashinda kwa matuta  5-4 dhidi ya Mwadui fc baada ya sare ya bao 2-2.



No comments

Powered by Blogger.