GARETH BALE APATA MTOTO MWINGINE.

Nyota wa Real Madrid na Nahodha wa timu ya Taifa ya Wales Gareth Bale amepata mtoto wake wa pili wa kike leo.



Bale kupitia ukurasa wake wa Instagram na Twitter  ameweka picha inayoonyesha ameshikwa kidole na mwanae huyo akiweka maneno yanayoambatana na picha hiyo " Leo Nina Furaha kumkaribisha Mrembo mwingine wa kike katika familia yetu. Nava Valentina Bale"

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 26 amerejea Uwanjani hivi karibuni akitoka majeruhi ya muda mrefu na hatokua pamoja na timu ya Taifa ya Wales katika michezo ya kirafiki dhidi ya Ireland Kaskazini na Ukraine kumpa muda wa kuwa na familia yake.

Jina hilo Nava linaaminika kuwa ni neno la Kiebrania lenye maana ya MZURI na ni mtoto wa pili wa Bale kwa mpenzi wake wa tangu utoto Emma Rhys-Jones na mtoto wao wa kwanza anaitwa Alba Viola ambaye alizaliwa Wales Oktoba 2012.



No comments

Powered by Blogger.