ZANZIBAR HEROES KUFUNGUA CHALLENJI LEO YAANZA NA BURUNDI

Kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar  ‘Zanzibar heroes’ tayari kipo Addis Ababa nchini Ethiopia  kwa mashindano ya Kombe la Chalenji yatakayoanza kutimua vumbi leo Jumamosi nchini humo.
Zanzibar Heroes wapo kundi B sambamba na Kenya, Uganda na Burundi.

Wachezaji waliosafiri na timu hiyo ni
Makipa: Mwadini Ali (Azam), Mohamed Abraham (JKU).
Mabeki wa pembeni: Mwinyi Haji (Yanga), Nassor Masoud (Stand United), Adaymu Saleh (Coastal Union) na Ismail Khamis (JKU).
Walinzi wa kati: Nadir Harub (Yanga), Shafii Hassan (Zimamoto), Said Mussa (Mafunzo), Issa Haidary (JKU).
Viungo: Awadhi Juma (Simba), Mudathir Yahya (Azam), Saidi Makapu (Yanga), Mohamed Abdulirahmani Mbambi (Mafunzo), Hamis Mcha (Azam), Suleiman Kassim (Stand United) na  Omari Juma (Hard Rock).

Zanzibar heroes  itacheza mchezo wake wa kwanza leo dhidi ya Burundi

No comments

Powered by Blogger.