CHELSEA YAZIDI KUGAWA POINTI LIGI KUU NCHINI ENGLAND


Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini England klabu ya Chelsea imeendeleza wimbi la matokeo mabaya msimu huu baada ya kufungwa bao 1-0 na Stoke City

Mechi hiyo ya ligi kuu nchini England ilipigwa katika dimba la Britania nyumbani kwa Stoke City ambao leo walikua katika kiwango bora kabisa.

Goli pekee la Stoke lilifungwa kipindi cha pili na mshambuliaji Marko Anartovic baada ya kutokea shambulizi kali lililofanywa na vijana wa Mark Hughes.

Kwa matokeo hayo Chelsea imebaki na pointi zao 11 katika nafasi ya 16 ikiwa ni nafasi mbili toka katika mstari wa kushuka daraja.

Katika mechi ya leo kocha Jose Mourinho hakuwepo kutokana na adhabu inayomkabili

No comments

Powered by Blogger.