KINACHOWATISHA WAPINZANI WA MAN UNITED NI "SAMSUNG GALAXY S2"


Bastian Schweinsteiger afaulu vipimo vya afya kujiuinga na klabu ya Manchester United kukiwa na habari za uhakika kutoka skysports ya kwamba Morgan Schneiderlin yupo njiani kujiunga na Manchester United.. Hii ilikua siku mbaya ambayo iliuchoma moyo wa Arsenal Wenger pamoja na Jose Mourinho. Ilikua ni siku ambayo Samsung S2 Galaxy inazinduliwa rasmi. Schweinsteiger and Schneiderlin.

Wakati nikiwa mdogo niliambiwa kwamba sauti yako ikianza kubadilika na kuwa tofauti ya awali jua kwamba umekuwa. Yoyote anayekuzungumzia juu yako ni kutokana na mabadiliko, mwenendo na tabia yako nzuri uliyojijengea tangu awali. Baba mzazi anapofariki kisha Mama Mzazi kuamua kutafuta Baba mwengine wa kambo daima huwa ni kipindi kigumu cha mtoto. Mtoto anakua anajifunza maisha mapya ya Baba mwengine na pia Baba huyu naye ujifunza maisha mapya ya kumfahamu mtoto na kisha kumjenga misingi ile aliyokuwa akiipata kupitia kwa Baba mzazi.
Note; Baba Mzazi ni Alex Ferguson, Baba wa kambo ni Louis Van Gaal na mtoto ni Manchester United.

Ni lazima kuwe na muda wa kuzoeana kwa kutenganisha zege la matabaka katikati ya shina la uvumilivu, upendo, thamani na uchapakazi.. Sir Alex alifia mikononi mwa mtoto kisha LVG akavaa kiatu cha mtoto. Ni jukumu lake kumvalisha na kumfanya mtoto aendelee na safari yake. Safari ambayo kwa asilimia kubwa Baba wa kambo ameianza vizuri.

Wengi tunafahamu mfumo aliokuja nao Louis Van Gaal ni wa kuijenga timu na kurekebisha mapungufu yote yaliyokuwa yakizibwa kutokana na uzoefu wa Sir Alex. Pengine naweza kusema uchawi wake au kipaji alicho nacho kilichomfanya amuaminishe kwamba Wes Brown anfaa acheze fainali ya Champions League 2008 au Fabio da Silva alikua akistaili kumkaba Lionel Messi wakati wa fainali pale Wemblay. Haya yalikua moja yupole wa mapungufu ya United yaliyokuwa yakizibwa na kocha mwenye kipaji Sir Alex. Inapotokea kocha mpya kisha akayafumbia macho upole wa twiga ndio kinamkuta mkimbizi aliyekosa muelekeo Mr Moyes.

Shukrani zimuendee Louis Van Gaal kwa kuweza kuicontrol na kisha kujenga falsafa zake. Falsafa zilizotawala ubabe, ukweli na uchapakazi. Mtoto daima uanza maisha magumu anapojaribu kuanza maisha mengine upya. LVG ameitengeneza United katika falsafa anayoitaka yeye katika msimu wake wa kwanza. Falsafa iliyokuwa ikihitaji muda kuweza kuona matunda yake. Pengine naweza kusema matunda haya yanayoanza kujitokeza yanachangiwa na povu la sabuni linalotoka bila kufikichwa. Povu la mpinzani.

KAULI-- MANCHESTER UNITED WANANUNUA UBINGWA.
Majuzi Arsenal Wenger alikuja na kauli ya dhiaki huku akisema mbele ya vyombo vya habari kuwa Louis Van Gaal ananunua Ubingwa kwa usajili alioufanya. ameweza kutumia kiasi cha Pound mil 80 kwa wachezaji wanne tu huku yeye akitumia Pound mil 10 kwa mchezaji mmoja. Jana Jose Mourinho naye akasema kwamba Manchester United wananunua ubingwa. Kauli moja kupitia makocha wawili tofauti kutoa lawama mbele ya umma.

UTHIBITISHO
Siku zote unapofanya usajili wa dirisha kubwa mara nyingi unakuwa unajipanga kwa msimu mzima wa ligi kuu, mara nyingi unakuwa unajiwek vizuri either kwa ubingwa au kujiweka kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa kigi. Inapotokea ukafanya usajili wa dirisha dogo la January hapo unakuwa tayari umeshajiwekea malengo yako thabiti jinsi utakavyoweza kumaliza ligi. Pengine hapa ndio sehemu unayoweza kusema timu flani inanunua ubingwa.

Msimu uliopita Chelsea ikiwa bado inaongoza Ligi Kuu Ya Uingereza huku ikielekea kuonesha kulibeba still ilitumia kiasi kingi cha pesa cha Pound mil 27 kumnunua Juan Cuadrado. Mwezi huo huo mwenzake Arsenal Wenger naye akatumia kiasi cha Pound mil 15 kumchukua Gabriel Paulista kutoka Virrareal huku wakiwa wamejisahau kama walitumia kiasi cha pesa kuwanunua Diego Costa, Fabregas pamoja na Alex Sanchez.

UKWELI.
S2.... Samsung S2 ndio ukweli wa majibu yote. Hii ndio nafasi ambayo United ilikua ikipoteza pindi ambapo Michael Carrick alikua majeruhi. S2 ya Schweinsteiger na Schneiderlin imefanya kuziba pengo ili kisawasawa. Muangalie Schneiderlin anavyokaba pale kati kwa umakini kisha chuku uzoefu wa Schwinsteiger na pasi zake za box to box utagundua kabisa hii ndio sehemu ambayo sindano ya LVG imewafanya Mourinho na Wenger watokwe mapovu.

Pengine labda wamegundua kipaji cha Darmian cha kutumia miguu yote kama beki au skills za Depay anavyowaburuza wapinzani.. Lakini kocha yoyote proffesional hawezi kusimama mbele ya waandishi wa habari na kutoa kauli za kusema timu flani inanunua ubingwa ikiwa ushahidi wako wa kumkamata panzi na na kusema akutetee huku ukijua muda wowote atakuruka.

Kocha profesional anayejitambua ni yule anayekubali matokeo. Luis Enrique baada ya kupata kipigo cha mabao 3-1 amekiri kwamba United ya sasa ina uwezekano mkubwa wa kubeba makombe matatu kama alivyofanya yeye msimu uliopita akiwa na Barcelona. May be naweza kusema ametumia kauli ya kiproffesional kama kocha.

KWA MASHABIKI WA MAN UTD.
Usitetereke na habari zozote zinazoendelea kwa sasa juu ya Di Maria au De Gea. Siwezi kumsema Di Maria kwa kiwango chake au kuzungumzia ubora wa De Gea. Lakini nawaomba jicho la tatu tulitupilie kwa Samsung S2. Tumeweza kupata S2 na hii ndio ilikua sehemu kubwa tuliyokuwa tukihitaji. Unapokuwa na watu kama Bastian au Morgan kisha ukawa na Carrick au Herrera daima utajilingia kubalance mbele na nyuma.

Raktik ndie alikua man of the match fainal ya Uefa msimu uliopita na alisaidia barca kwa kiasi kikubwa kubeba makombe matatu kama kiungo cha kati. Matic aliibeba Chelsa, Pogba Juve, Alonso Bayern na ata ubora wa Carzola dk za lala salama kuliifanya Arsenal kushinda mechi nyingi za mwishoni. Viungo ndio wananunua ubingwa.

Karibu sana S2 naamini Baba wa kambo sasa anaanza kumjenga mtoto vizuri kwenye misingi ile ile aliyopitia kutoka kwa Baba Mzazi. Pengine Jose na Arsene wanajua hii ndio sehemu tuliyonunua ubingwa japo hawataki kuweka wazi. Lakini Je tuwaulize wao wanaponunua kipa Petr Cech miaka 34 kwa kiasi kingi cha Pound mil10 au Mourinho kumtaka Stone wa Everton kwa Pound 25ml baada ya awali Pound mil 20 kukataliwa je wao wananunua mchicha??


‪#‎WelcomeSergioRomero‬

~ By David Peter Herrera

No comments

Powered by Blogger.