SIMBA NA AZAM MBIO ZILE ZILE LIGI KUU BARA


Licha ya ushindi wa bao 3-0 walioupata Simba SC leo dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara Nafasi ya pili katika ligi kuu Tanzania bara imezidi kuwa ngumu kwao baada ya Azam kuibuka na ushindi wa bao 4-0 wakiifunga Stand United ya Shinyanga.

Shujaa wa mchezo kati ya Azam na Stand alikua mkongwe Gaudence Mwaikimba aliyefunga mabao mawili peke yake huku Brian Majwega na Faridi Madiki wakifunga bao moja kila moja ikiwa Azam nafasi ya kuendelea kutamba katika nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 45.

Kwa upande wa Simba wao wameibamiza Ndanda FC bao 3-0 magoli ya Said Ndemla,Jonas Mkude na Ramadhani Singano ushindi ambao umeongeza pointi kwa Simba na kufikia pointi 41 katika nafasi ya 3.

Yanga wao wanazidi kuongoza ligi wakiwa na pointi 50 ikiwa ni pointi 10 mbele ya Azam FC wanaokamata nafasi ya pili.

×××××××××××××××××××××××××××

No comments

Powered by Blogger.