●● INSIDE UNITED●●.JEZI YA DI MARIA YAKIMBIZA KATIKA CHATI WAMO PIA DE GEA, ROONEY,FALCAO NA VAN PERSE.

..
Leo katika INSIDE UNITED tunaangalia mauzo ya jezi za Wachezaji ambazo hizo huwa ni kati ya vyanzo vya mapato ya klabu.

Licha ya kuonekana kiwango chake kushuka katika siku za hivi karibuni winga wa Manchester United Angel Di Maria ameongoza kwa mauzo ya jezi zenye jina lake ambapo katika wastani wa watu 10 wanaonunua jezi angalau mmoja hutaka kuandika jina la Angel Di Maria katika mgongo wake.

Winga huyo ambaye alisajiliwa kwa paundi milioni 60 akitokea Real Madrid ameongoza kwa jezi yenye jina lake kuuzwa zaidi ya mchezaji yeyote katika ligi kuu nchini England na hizi ni takwimu zilizotolewa na wauzaji wa vifaa vya michezo SPORTS DIRECT ambao huuza jezi za Aston Villa,Chelsea,Liverpool, Arsenal Man United,Man City,Totenham na Newcastle United.

Katika orodha ya 10 bora wachezaji watano wanatoka katika klabu ya Manchester United ambao Ukiacha Angel Di Maria wamo pia,David De Gea,Wayne Rooney, Radamel Falcao na Robin Van perse.

ORODHA YA WACHEZAJI WANAOONGOZA KATIKA ORODHA.


1. Angel Di Maria
2. Alexis Sanchez
3. Diego Costa
4. David De Gea
5. Eden Hazard
6. Wayne Rooney
7. Radamel Falcao
8. Steven Gerard
9. Sergio Kun Aguero
10. Robin Van Perse

Kwa leo ni hayo tu ila usikose kuwa shuhudia wachezaji wa United leo wakiziwakilisha timu zao za Taifa katika mechi mbalimbali ikiwemo mechi ya kirafiki kati ya Italia dhidi ya England ambapo United itakua na Rooney,Carick,Phil Jones na Smalling.

ENJOY

No comments

Powered by Blogger.